Uzoefu na matumaini njiani mwa ushirikiano

Muhimu kwetu ni kwamba watu wenye mila na desturi tofauti ambao ni wafuasi wa dini moja wawe na nafasi ya kuweza kuonana. Katika mwaonanano huo tunapata ujuzi juu ya tofauti hizo katika maisha ya kiuchumi na kimila. Tunawasiliana katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili. Tunakutana katika aina nyingi, kwa mfano wa kuimba, kufanya kazi pamoja, kutembea tembea. Tunaelimishana sisi kwa sisi, tunasali pamoja. Tunashirikishana maisha yetu katika familia na shirika zetu na vikundi vyetu.

Kwa wakati huu tunasaidia katika ujenzi wa hosteli ya kikundi cha wanawake Tukuyu.
Haja ya kipekee kwetu ni kazi ya Akina Mama wafanikiwe. Katika wajibu wao tunawasaidia hasa kuuimarisha mradi wa yatima. Katika mradi huu yatima wanatunzwa vizuri sana katika familia mbali mbali za waumini.