projects-aidsorphans-02

2015

Visitor Group 2015 in Tukuyu

I

likuwa kundi la wageni wa shirika na jumuiya ambazo hujitolea kwa ushirikiano. Kuna wajumbe wapya wa kamati ya ushirikiano wa Tukuyu. Mikazo ya miradi ndiyo mipya.


2013

2013

N

a wageni kutoka Tukuyu tuliamua katika mazungumzo wazi sana pamoja, kwamba sisi itakuwa kuwasilisha ushirikiano wetu kwenye tovuti na taarifa ya sasa ya Tukuyu na Ulm katika siku zijazo. folder mpya itaonekana na taarifa ya sasa.


2011

2011

M

iaka 30 ya ushirikiano tunasherehekea wakati wa mwaka huu siyo katika shirika zetu za kanisa hapa Ulm tu lakini pia kwa kundi la watembeleaji 12 pale Tukuyu. Kuvutia hasa ni maadhimisho huduma katika kanisa Tukuyu


2009

2009

K

wa muda mrefu wa ushirikiano wetu tulipata wakati wa ziara kutoka Tukuyu thamani pekee katika mikutano yetu yote: upendano, moyo wa uwazi na kuwa na moyo wa kukosoana.


2007

2007

M

ikutano ya vijana na mazungumzo juu ya vichwa mbali mbali kama vile „ujana na kanisa“, „afya“, „haki duniani“ yalikuwa na mkazo mkuu katika ziara ya wajumbe wa Ulm huko Tukuyu. Mwanzoni kundi la Ulm lilikaa katika „nyumba ya wageni“, baadaye wageni walikaribishwa katika nyumba za waumini.


2005

2005

W

akati wa safari ya tano ya wajumbe kutoka Tukuyu, wageni hao walipata nafasi ya kuonana na watoto pamoja na vijana katika mikusanyiko yao na pia katika Shule zao kufundisha masomo ya Kipa Imara. Tuliongea kuhusu njia ya kuwapa vijana nafasi ya kujiunga na makundi ya kutembeleanai.


2003

2003

T

ulipata nafasi ya kuongea vizuri na kwa uwazi na makundi yote ya ushirika. Mazungumzo haya yalikuwa muhimu sana wakati wa safari hii ya tano ya wajumbe kutoka Ulm kwenda Tukuyu.

2001

2001

W

ageni kutoka Tukuyu walipotutembelea kwa mara ya nne mambo muhimu katika ziara hiyo yalikuwa kuhudhuria mkutano mkuu wa makanisa ya kilutheri ya Ujerumani huko Frankfurt, majadiliano maalum katika nyumba ya starehe „Schlössle Erbstetten“, kusherehekea miaka ishirini ya ushirikiano.


1999

1999

K

wa mara ya nne kikundi cha watu kutoka jumuia zetu tano walitembelea Tukuyu. Ziara hii ilikuwa ni mara ya kwanza katika matembeleano kupata malazi katika familia za waumini.


1997

1997

K

wa mara ya tatu washiriki sita kutoka Tukuyu walikuwa wageni wetu. Na kipeo cha safari hii kilikuwa mkutano mkuu wa makanisa ya kilutheri ya Ujerumani (Deutscher Evangelischer Kirchentag) huko Leipzig na ziara kwa wafuasi wa „Brüdergemeinde“ huko Herrnhut.

1995

1995

W

akati wa ziara ya tatu ya wageni kutoka Ulm waliweza kualikwa pia na shirika za Makandana, Ndembela na Lumbila ambazo zinajitegemea na ushirika wa Tukuyu sasa.


1993

1993

W

akati wa ziara ya pili ya wajumbe wa usharika wa Tukuyu, uhusiano baina ya waumini na kati ya jumuia hizi mbili umeimarika. Tulikuwa kualikwa 1995 kwenda Tukuyu.

1991

1991

K

wa mara ya pili wajumbe wa jumuia za Ulm walitembelea Tukuyu. Mwaka huo huo pia mradi wa ng´ombe wa waziwa ulianzishwa


1989

0

B

aada ya Mchungaji Hauff kurejea kutoka Chuo cha Theolojia alifanya kazi katika usharika wa Dornstadt. Waumini wa Dornstadt waliamua kujiunga na ushirikiano.

1988

1988

W

awakilishi sita wa kikundi cha vijana wa Tukuyu walitembelea jumuia za Ulm kwa muda wa wiki nne.


1986

1986

M

wanzoni ushirikiano ulikuwa hasa kati ya kikundi cha vijana wa Wiblingen na wajumbe wawakilishi wa jumuia hizo. Mwaka huo huo vijana sita toka jimbo la kidini la Ulm walitembelea Tukuyu kufuatia mwaliko wa kikundi cha vijana wa Tukuyu.




1981

0

M

chungaji Mwakasyuka toka Tukuyu alitambua bidii ya waumini wa jumuia za Ulm, ili kuunda ushirikiano kati yao na kanisa la Moravian Tukuyu – Tanzania.